Tuesday, May 10, 2016

RASMI: KESSY ATIA DOLEGUMBA YANGA

Kuna msemo wa Kiswahili unasema ‘ukisusa wenzio wala’, msemo huu umetimia baada ya beki wa kulia wa kikosi cha Simba SC Hassan Kessy kutia dolegumba kwenye fomu za usajili za Yanga na kujiunga na mabingwa hao wa mitaa ya Twiga na Jangwani.

Kessy ametia saini juzi mkata wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Yanga kwa miaka miwili kuanzia mwezi ujao (June, 2016).

Awali Kessy alikuwa akiitumikia klabu ya Simba kabla ya kufungiwa mechi tano na wekundu hao wa Msimbazi kwa madai ya kuigharimu timu kutokana na kitendo cha kuoneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Toto Africans mchezo uliomalizika kwa Simba kupoteza kwa bao 1-0.

Licha ya Simba kumfungia Kessy, tayari beki huyo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba ns kupandisha mashambulizi mkata wake wa na Simba unamalizika mwisho wa msimu huu na klabu hiyo haikuonesha nia ya kuhitaji huduma ya nyota huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar.