JE WAJUA?
George Junius Stinney, Jr. Ndiye kijana mdogo Mwenye umri wa miaka 14, ndiye aliyehukumiwa kifo kwa kiti cha umeme mwaka 1944 baada ya wasichana wawili wa kizungu , miaka 11- Betty June Binnicker na Miaka 8- Mery Emma Thames kupotea na miili yao kuokotwa kesho yake ikiwa tayari wamekufa na mtu wa mwisho kuonekana akiongea na hawa watoto alikuwa ni huyu kijana mwenye asili ya afrika - George(14).
Kesi hii ilikuwa batili maana mashahidi wa kesi hii walikuwa polisi waliosema George amekiri shitaka(confess) ila hapakuwepo na maandishi(records)yoyote ya kuonyesha kukiri kwake.
Polisi wawili na madaktari walioenda eneo la tukio na madaktari kuifanyia miili postmortem. Polisi na madaktari hawa walikuwa wazungu.
Kesi hii ilichukua siku moja , jopo la majaji lilikuwa ni wazungu pekee kwasababu kipindi hicho BLACKS hawakuruhusiwa kupiga kura(right to vote), Goerge alibaki pekee yake bila shahidi kwasababu alikuwa mweusi(black).
Kesi ilichukuwa masaa mawili na kumhukumu George hukumu ya kifo kwa kukaa kiti cha umeme.
Wakati anawekwa kwenye kiti cha umeme ilikuwa ni taabu kidogo kwani George alikuwa na urefu wa sm 155 na uzito usiopungua pounds 90 (40kg) kutokana na umbile lake dogo code ya umeme ilikuwa taabu kutoa umeme.
Hivyo, George akawekewa mfano wa sufuria kichwani na akavikwa mask ya umeme kisha apigwa na shot ya umeme yenye nguvu ya 2400V kutokana na udogo wa kichwa chake mask ilifumuka na kuonesha fuvu lake likiwa wazi, midomo akitokwa na mate na machozi machoni.
Wakapiga shot nyingine George akawa amefariki....baaba ya kufariki mikanda aliyokuwa amefungwa mikononi. Mkono mmoja wa kushoto ulikata mkanda kuashiria alikufa kifo cha kinyama....
RIP George Junius Stinney, Jr (14).
No comments:
Post a Comment