Thursday, April 7, 2016

Facebook yatumika kuuza silaha Libya

Utafiti mpya umebaini kwamba kuna soko linaloendelea kuimarika
katika biashara haramu ya bunduki nchini Libya kupitia mitandao
ya kijamii hususan ule wa Facebook.
Ripoti hiyo inayoangazia miezi 18 ilibaini mauzo ya vifaa vingi
kutoka bunduki hadi makombora ya kutungua ndege.
Vifaa hivyo vilikuwa vikiuzwa kupitia mitandao ya siri ya makundi ya
Facebook.
Uuzaji wa bunduki ni ukiukaji wa sheria za huduma ya mtandao huo
na msemaji wa Facebook amesema kuwa wanawataka watu kuripoti
kuhusu machapisho kama hayo.
Ripoti hiyo ilizinduliwa na utafiti wa silaha ndogo ndogo na data
iliochunguzwa na shirika la utafiti la Armament katika mauzo 1,346.
Watafiti wanaamini kwamba hicho ni kipande kidogo cha biashara
yote inayoendelea katika mitandao ya kijamii.
Utafiti huo utatolewa siku ya Alhamisi,lakini BBC Newsnight inasema
inamiliki nakala ya utafiti huo.
Kanali Muamar Gaddafi alikuwa mnunuzi mkubwa wa silaha na
alidhibiti soko la silaha.
Katika kipindi cha miaka 40 alichokuwa mamlakani,inakadiriwa
alitumia dola bilioni 30 kununua silaha.

No comments:

Post a Comment