Friday, April 8, 2016

KISWAHILI KWA WANAFUNZI: Ngeli tisa za Kiswahili na upatanisho wa kisarufi

Kwa ufupi
Kufahamu ngeli za Kiswahili kunamwezesha
mwanafunzi kuelewa upatanisho wa kisarufi
katika sentensi, kutambulisha maumbo ya umoja
na uwingi pia kufahamu uhusiano wa Kiswahili
na lugha zingine.
Habari
TUESDAY, JULY 22, 2014
KISWAHILI KWA
WANAFUNZI: Ngeli
tisa za Kiswahili na
upatanisho wa
kisarufi
 13   0  0  0
 0  0  13
Ngeli ni vikundi vya majina ya Kiswahili. Ngeli za
nomino ni utaratibu unaotumika kuweka nomino
katika matabaka au makundi yanayofanana.
Kufahamu ngeli za Kiswahili kunamwezesha
mwanafunzi kuelewa upatanisho wa kisarufi katika
sentensi, kutambulisha maumbo ya umoja na uwingi
pia kufahamu uhusiano wa Kiswahili na lugha
zingine.
Ngeli ya A–WA hutumika kurejelea viumbe vilivyo
hai (wanyama na watu). Majina mengi katika ngeli
ya A-WA huanza kwa sauti M- kwa umoja na sauti
WA- kwa wingi. Hata hivyo baadhi ya majina
huchukua miundo tofauti.
Mifano; mgonjwa - wagonjwa, mchungaji -
wachungaji, mwizi-wezi, mtu- watu.
Muundo ulio tofauti na maelezo hapo juu ni kama
mbuzi-mbuzi, kwale - kwale, nyati - nyati
kifaru – vifaru.
Ngeli ya LI-YA husimamia nomino zenye miundo
mbalimbali. Licha ya majina ya vitu visivyo hai,
ngeli hii pia hutumika kwa majina yote katika hali
ya ukubwa (yakiwamo ya watu au wanyama).
Majina mengi huanza kwa JI- au J- kwa umoja na
hubadilishwa kuanza na MA- au ME- kwa wingi.
Majina mengine ambayo huanza kwa sauti nyingine
kama vile /b/, /d/, /g/, /k/, /z/ n.k ambayo huwekwa
katika wingi kwa kuongeza kiungo MA-
Mifano; jimbo - majimbo, jicho - macho, jiko -
majiko, jino - meno, maua, umbo - maumbo, bati -
mabati.
Ngeli ya KI - VI hurejelea vitu visivyo hai ambavyo
majina yao huanza kwa KI- au CH- (umoja) na VI- au
VY- (wingi).
Mifano; kijiko - vijiko, kikapu - vikapu, kioo- vioo,
choo - vyoo, chumba - vyumba, chuma - vyuma,
chungu - vyungu
Ngeli ya U - I huwakilisha nomino za vitu visivyo hai
na ambavyo majina yake huanza kwa sauti M -
(umoja).
Mifano; mfupa - mifupa, mtambo - mitambo, mfuko
– mifuko.
Ngeli ya U - ZI hurejelea majina ambayo huanza kwa
U- (umoja) na huchukua ZI- kama kiambishi
kiwakilishi cha ngeli katika wingi.
Mifano; ufunguo - funguo, ukuta – kuta.
Majina ya silabi mbili katika ngeli hii huongezwa NY
katika uwingi. Mifano; uzi - nyuzi, uso – nyuso.
Ngeli ya I - ZI hutumiwa kwa majina yasiyobadilika
kwa umoja wala kwa wingi lakini huchukua
viambishi viwakilishi tofauti: I- (umoja) na ZI-
(wingi). Aghalabu haya ni majina ya vitu ambayo
huanza kwa sauti N, NG, NY, MB, n.k
Mifano; nyumba - nyumba, nguo - nguo, mbegu -
mbegu, nyasi - nyasi, nyama – nyama.
Ngeli ya U - YA hujumuisha nomino ambazo zina
kiambishi awali u-katika umoja na ma- katika
uwingi.
Mifano; unyoya - manyoya.
Ngeli ya KU huwakilisha majina yanayotokana na
vitenzi kwa vitenzi vinavyoanza na ku-(huitwa
vitenzi jina). Mfano Kusoma kwetu kumetusaidia,
Kusema uongo kumemponza.
Ngeli ya mahali PA - KU – MU. Ngeli ya PA hurejelea
mahali maalumu, padogo au palipo wazi. Ngeli ya
KU hurejelea mahali fulani kwa jumla au eneo
fulani. Ngeli ya MU - hutumika kurejelea mahali
ndani ya kitu kingine kama vile ndani ya nyumba,
shimo n.k. Ngeli za mahali hubaki vivyo hivyo katika
umoja na wingi
Hivyo, mwanafunzi anaweza kufanya mazoezi kadiri
awezavyo kwa kutunga sentensi umoja na uwingi
kwa kutumia neno au kitenzi jina ili kubaini kundi
husika la neno au maneno.
Mwandishi ni mtaalamu wa Kiswahili.

No comments:

Post a Comment