Thursday, April 7, 2016

Ni haramu kulipia ngono Ufaransa

abunge nchini Ufaransa wamepitisha mswada ambao
unaharamisha watu kulipa ili kupata huduma ya ngono na kuweka
faini ya hadi dola 4,274 kwa wale watakaopatikana na hatia.
Wale watakaopatikana na hatia pia watalazimika kupewa mafunzo
ya mazingira yanayowakabili makahaba.Imechukua zaidi ya miaka
miaka miwili kupitisha mswada huo wenye utata kutokana na tofauti
zilizopo kati ya mabunge mawili kuhusu swala hilo.
Baadhi ya makahaba waliipinga sheria hiyo wakati wa mjadala wa
mwisho.
Waandamanaji 60 walipiga kambi nje ya bunge mjini Paris, walibeba
mabango moja likiwa na maandishi yaliosema:''Sina haja ya
kukombolewa, nitajikomboa mwenyewe'',kulingana na chombo cha
habari cha AFP.
Muungano wa makahaba wa Strass umesema kuwa hatua hiyo
itaathiri maisha ya kawaida ya makahaba wanaodaiwa kuwa kati ya
30,000 na 40,000.
Lakini wanaounga mkono sheria hiyo wanasema itasaidia
kukabiliana na mitandao ya ulanguzi wa binaadamu.
Pia itakuwa rahisi kwa makahaba wa kigeni kupata kibali cha
kufanyia kazi kwa mda nchini Ufaransa iwapo watakubali kutafuta
kazi zisizo za ukahaba.
Umuhimu wa sheria hiyo ni kushirikiana na makahaba ,kuwapatia
vibali vya utambuzi kwa sababu tunajua asilimia 85 ya makahaba ni
waathiriwa wa ulanguzi wa binaadamu ,mbunge wa chama cha
kisosholisti Maud Oliver ambaye alifadhili sheria hiyo aliambia
chombo cha habari cha AP.

No comments:

Post a Comment